Shaka!

The Bee.

Mi nilimshow.Mi nilimshow hao wadhii ni wazii but akanishow zii:ye ndo fastbodii Koch, Kibich,Mukuru na Huruma na ye ndo kusema.Nilitry kumshtua wasee kadhaa walikuwa wamededi juu ya kudeal na hiyo mbogi na kumess mless tu but akanishtua ati kaa Corona imemtii hiyo mbogi watamweza kweli?Ah,si hiyo reba ikadie.Saa si tumetulia tu.Kiasi kiasi tunaskia sauti kaa ya kibomb bomb hivi;sisi nani? Si tumeingia chini ya bed.Si nakushow mlango haijavunjwa ikaanguka!Mi nilicheki tu viatu fulani bigi kadhaa nikajua tu tumeisha.

Kaa Sir God alikuwa huko juu ingebidi saa ameshuka na asitumane.Si bado tuko apo tumetetemeka design ya ingoho imenyeshewa tunaombwa tusipatwe.Ndo hiyo baze fulani ikaongea…..

‘Oyaa saa ni hivi, tunasaka jamaa anaitwa Shaka.Msitubebe ufala! Tunajua mko apa na kabla tucheze brikicho na nyi mtokee tu.’

Idhaa inasonga. Hatutokei. Sijakwambia bed ikainuliwa hatujajipata tukiangaliana na ponye.Si tumeshindwa kupumua.Shaka ameshikwa mashati ameinuliwa kaa feather za kuku na mi naskia manduru mingi mingi kumbe sauti ni yangu.Bana joh mi si niko apo nmelia nmetetemeka hadi hao mapai wakanishow si mimi wanachukua.Wakaenda na Shaka tu hivyo wakamwingiza kwa black maria akiniangalia na macho za uwoiye kaa dogi imenyimwa mbinginji.

Kitambo vitu hazikuwa hivi msee.Kitambo mi na bro wa mine, Shaka,tulikuwa fiti.Tulikuwa na wazae,na buda na masa,na tulikuwa mabombe tunaishi kwa hao fulani bigi Kile.Tulikuwa tunadishi mara kaa saba kwa siku na hatukuwai kuwa na shida ya kukosa keroma ata day moja.Life ilikuwa fiti mbaya na tulikuwa tunaendanga chuo fulani praivet.But saa juu fate si shosho ya mtu si mapero wetu walienda uko juu wakakuwa malaika.Kaa unawatchingi muvi za Naija unajua tu mapero wakidedi watoto huenda kuishi na anti yao mbaya mwenye huwatesa na huwanyima food na huwakataza kwenda shule.Saa si stori yetu ilikuwa hivyo.

Tulikaa huko miezi kadhaa tukaona hatuwezi endelea hivyo tukahepa.Saa hizo days Shaka alikuwa miaka 16 na mi nilikuwa 12.Tulitorokea Kibich na mara za first tulikuwa tunauza njugu na tropkos kwa rodi hapo Mbagathi kwa jam na kwa siku tungepata kaa rwabe enye tulitumia kusakia keroma na kubai screp ya kumaliza maliza hao yetu enye tulikuwa tumeekelea mbao fulani na kajuala.Venye idhaa ilisonga nikacheki Shaka alikuwa anatoka kabla jua itoke na anarudi ikishaingia.Nikamshow asijione mzii:atulie achengwe juu ata hatukuwa tumekaa hii mtaa sana.

Si nakushow beshte yangu Paipu akanishtua ati bro mine hupiga watu ngeta na kuwatoka doh na tenje.Mi sikuamini.Ndo maana siku hizi tulikuwa tunadishi fiti.Ndo maana tulihama kwa keja ya mabati ya soo tano.Ndo maana alikuwa ananiuliza kaa ningetaka tukuwe na mbulu.Nilikuwa nmechezwa. Nilidhani ati amepata janta fiti kumbe alikuwa thegi.Saa ningedo? Hakuna.Nikamshow haina ile bora asipatwe acheze kiyeye.Juu mi sikuwa nadai ngori na mapai.Akasema ye ndo ule msee, mkali wao na hawatampata:ati wangemkuta angewasho ye ni Bruce Lee mwenyewe.

Saa si day fulani Shaka akafika kejani na nyama kg moja na sembe ingine bigi kaa anacheka cheka akinishow,

‘Sistee life yetu itakuwa fiti sana.’

Sikuwa nmemcheki amefurahi hivyo siku mob sana saa si pia mi nimechangamka nmechapa kasmile.Nikamwambia afanye chwaka anishow.Akanishow amepata deal fiti ya kuuza vitu Blak maket na rende ya wasee walijiita ‘Weusi’.Wacha mi sijashtuka.Hii genge nilikuwa nmechapiwa reba na Paipu walikuwa wanaua wasee kaa kuku wakimess.

Si ndo nikamwarn but mapai wakamkujia. Siku hizi naishingi tu kimungu mungu juu ata mi wakinikamia sijui ntaanzia wapi.Ebu chill kiasi. Naskia kelele ya gari.Nachungulia nacheki ni Black Maria.Washakam na brathangu?Bana joh ule Shaka alitolewa si ule nilikuwa najua.Msee amepigwa wamemchafua ata macho moja haifungi.Wakaniambia nisonge kando na Shaka akaambiwa ainue mikono aniangalie.Kiasi kiasi si ponye mmoja ametoa bastola.Mi na nduru zangu nalia wasimuue.’Dush nyau.Dush nyau. Dush nyau.’Hivyo ndo walimdedisha.Si ndo huyu mimi namshikilia siamini ameenda. Saa ningedo?Haa,Shaka(venye DJ Shiti huisema)! Kwisha mimi!

The Bee.

One thought on “Shaka!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s